invité_SW

Soumis par derick le lun 22/04/2024 - 07:47

JUSTICE_ PRISON WALIKALE

Mratibu wa shirika  Bureau d’Etude et d’Appui au Développement de Walikale anatahadharisha wakuu viongozi kuusu  hatari inayoletwa na wafungwa wa kijeshi wanao kuwa ndani ya gereza kuu la mtaa hio. Obedi Kamala anasema hivi kwa sababu ana hakika kwamba gereza hii haieneze tena masharti ya kulinda vizuri wafungwa.  Anazungumziya hasa seli zisizo na milango tena. Kulingana naye, hali hii imedumu karibuni miezi sita tangu wafungwa wamoja wa kijeshi waliendesha fujo kali hadi kubomowa milango ya gereza kwaku dai malipo yao. Mtetezi huyu wa haki za binadamu anaeleza kwamba wengi kati ya wafungwa hawa wanabaki gerezani kwa utashi wao kwani hakuna kinachowazuia kutoroka. Hata hivyo, anatambua juhudi za viongozi kwa kulinda gereza hii lakini anadhani kuwa ni lazima kutenda mengi zaidi.

Audio

Ajouter un commentaire

HTML restreint

  • Balises HTML autorisées : <a href hreflang> <em> <strong> <cite> <blockquote cite> <code> <ul type> <ol start type> <li> <dl> <dt> <dd> <h2 id> <h3 id> <h4 id> <h5 id> <h6 id>
  • Les lignes et les paragraphes vont à la ligne automatiquement.
  • Les adresses de pages web et les adresses courriel se transforment en liens automatiquement.